Jinsi ya Kuchagua Kitambaa cha Sofa

Je, samani zako za ndani zilizopambwa vyema zinahitaji kuboreshwa? Hebu tazama vitambaa bora kwa ajili samani za kila aina, kuanzia masofa mpaka viti vya kulia chakula kutoka WOP.

 

 

 

 

 

Vitambaa vya Upholstery kwa ajili ya sofa mpya au viti vidogo ni uwekezaji mkubwa—huna haja ya kutafakari mara mbilimbili miezi michache baada ya mzigo kufika mlangoni kwako. Chagua malighafi mbovu, upambane na kisiki cha madoa ya hatari katika vitambaa vyako. Fanya kosa katika chaguzi zako za rangi au sampuli, hapo tena chumba kizima kitashika adabu yake (au utazikunja kwa ajili ya kwenda kujazwa upya tena). Hivyo basi kabla hujachagua kitambaa chako kipya, endelea kusoma ili utambue kipi hasa kitafaa katika misingi ya ubora, starehe, na mtindo pia. Hii ni mifano ya namna ya kuchagua vitambaa vizuri utakavyofurahia kuwa navyo kwa miaka chungunzima.

Kwanza, Vitambaa vya Upholstery

hivi ni vipi?

Vitambaa vya Upholstery ni malighafi—ambayo ndani yake ina kitambaa, padding (aina ya malighafi ya vitambaa vyembamba vya kuvishia masofa), kufunga mikanda migumu inayokaa chini ya sofa (webbing), na springi—ambayo hujenga mfungasho mzuri wa viti, masofa, na samani nyingine. Mchakato huu ulianza tangu Zama za Kati na kuanza kupata umaarufu kwenye karne ya 17, 18, na 19. Kwa miaka mingi, malighafi za aina mbalimbali zimepata kutumika, viti vya farasi na nyuzi nyingine muhimu kwa ajili ya kazi husika. Vitambaa vya Upholstery ya kisasa hutumia springi za chuma na kutengeneza uimara mkubwa zaidi. Angali malighafi za ndani zinaweza zisionekane, zina utofauti mkubwa sana kwa vyovyote vile zinastarehesha. Na ijapokuwa kitambaa kinaweza-kubadilishwa muda wowote ule—na vingi vinahitaji kubadilishwa, itategemeana na kuchakaa kwake. Kwa kuchagua tabaka za ndani zenye ubora wa juu itasaidia kitambaa kudumu kwa miaka tele ijayo.

 

Mpindo (mshono) wa Kiswidi—chagua utakao na tutukutumia sampuli zake ndani ya siku 2-5 za kazi, hivyo basi utapata kujua kitambaa utakacho kabla ya kufanya maamuzi yako juu ya vitambaa vya Upholstery.

 

Namna Gani Unaweza Kuchagua Vitambaa Bora kwa Ajili ya Sofa Lako (au Kiti, au Besela la Kitanda…)

Wakati unanunua vitambaa  kwa ajili ya Sofa, wacha mahitaji yako yakuongoze, ushauri kutoka kwa wataalam ulimwenguni. “Kwanza, fikiria unavyoishi na nani atakayetumia vitu hivyo. Hili litakuongoza aina gani ya malighafi unatakiwa kuchagua. Unaweza kupenda mwonekano laini, lakini utaharibiwa haraka ndani ya nyumba aidha na watoto au wanyama wako vipenzi, paka na mbwa. Maeneo yenye msongamano mkubwa, kama vile familia au ukumbini, utahitaji vitambaa vigumu, wakati samani ambazo hazitumiki sana, kama vile makochi ya chumbani au mabesela, yanaweza kupendeza kwa kitambaa chochote kile.

Makosa makubwa ambayo watu huyafanya, si kufikiria kuhusu namna kitambaa au ngozi inaweza kudumu kwa muda mrefu. Ufikapo katika maduka ya WOISO ORIGINAL PRODUCTS yaliopo sehemu mbalimbali Tanzania, uliza maswali dukani ili kufahamu malighafi iliyotumika au inaweza kutumikaje, na namna ya kuzisafisha pale ukihitaji. Halafu fikiria tena kwa kiasi gani umejiandaa kukarabati ili kulinda kile ulichokichagua. Na ujiulize itaonekana vipi baada ya miaka mitano endapo utanunua vitambaa hivyo sehem nyingine wasiojali ubora?. “Je, bado utaendelea kuipenda ngozi yako kadiri inavyozidi kutengeneza mng’ao kila siku ya Mungu? Je, utapuliza upepo wa kuondoka taka za vitambaa vya upholstery yako kila siku? Je, utayafunika wakati ukiwa haupo au hautatumia chumba ili kuepuka mpauko unaotokea wenyewe kwa kuakisiwa na mwanga wa jua?”

 

Vitambaa vyote vinavyosambazwa na Woiso Original Products vinafaa-maishani, kwa maana ya kwamba vinaweza kuvumilia mikiki-mikiki yote ya watoto, majimaji yanayomwagika, na wanyama vipenzi ndani, yaani, paka na mbwa.

Vitambaa Bora vya Upholstery Vinavyofaa Nyumbani Ukiwa na Watoto na Wanyama Vipenzi

“Mimi na kaka yangu tumekua tukizuiliwa kuingia sebuleni; ilikuwa kwa ajili ya shughuli maalumu tu,” anasema mteja wetu mmoja. Leo hii, ijapokuwa, kuna malighafi nyingi za upholstery zinazoonekana kuwa na uimara fulani. “Kwa watoto na wanyama vipenzi—na pengine wapenzi wa mvinyo—tunapenda ulaini wa ngozi ya suede na uimara wa vitambaa vya nje-na-ndani,” alisema. “Vilevile sisi ni wapenzi wa makochi ya vitambaa vya uphostery laini. Japo ukimudu ngozi halisi ni bomba sana na imara—huna tena hofu juu ya kuchafua ama kuchunika, na ngozi halisi pia hupatikana Woiso Original Products.” Kama una nyumba yenye pilika, kaa mbali na vitambaa vyepesi, kama hariri, ambayo inaweza kuvutika na haina subira linapokuja suala la kuingia madoa.

Hiki kitambaa chepesi cha upholstery kinapendwa sana kwa jinsi kinavyozidi kuimarika na kuwa laini kadiri muda unavyozidi kwenda.

Jinsi ya Kuchagua Malighafi Stareheshi ya Upholstery

Kama watoto wakorofi na wanyama vipenzi hawakutii presha, unaweza kweli kujidai kwa uhuru wako. Angali kitambaa cha ndani (linen) kina uimara, kwa rangi za kung’ara haitoi kiwango kikubwa cha kudhibiti madoa kwa nyumba zenye watoto wasio na staha, kuwa na mwonekano mzuri baada ya kukaliwa sana. Kama una wasiwasi kuhusu gharama, siku zote unaweza kutumia vitambaa aina hii kwenye mito, ambapo baadaye inaweza kutolewa pindi tu uonapo bidhaa mpya inayotamba au kutumika sana.

 

Bado twafikiri rangi ya uaridi isiyong’ara inafaa zaidi ambayo mtu anaweza kuipenda milele.

Usisahau Kuhusu umbo au shape ya samani zako

Upate picha ya samani akilini wakati unachagua kitambaa. Kama unaboresha fanicha yenye kona na mikunjo mingi, ni bora kuchagua vitambaa vyenye rangi moja, kwa kuwa ukichagua vitambaa vyenye maua au urembo wenye mwelekeo au mpangilio fulani, huenda ukaharibu mpangilio wake katika kukata vipande vipande vitakavyotumika kurekebisha sofa lako. Sampuli ya kitambaa inayoonekana vyema haiwezi kupendeza tena mara tu inapokatwa na kurudishwa tena katika sofa lako, hasa kama vile vyenye utata, hasa umbo la mapambo. Kumbuka kufahamu ukubwa wa samani zako pia. Tunapenda vipande vikubwa, kama vile vya sofa, ukipenda vile vyenye rangi za kupendeza au klasiki, kamwe hutovichoka daima. Kupendezesha kwa vipande vidogo—mathalani, kiti cha kukalia mtu mmoja kwenye pindo nene au embamba au hata bombwe. Tafakari kuhusu samani nyinginezo zilizomo chumbani—hasa zile zenye vipande vya vitambaa. Utatakiwa kuhakikisha rangi, msokotano wa umbile asili, na bombwe au sampuli yake zinaendana.

Uwe na uhakika na umakini kutopoteza marembo au chapisho za vitambaa vya rangi ya mchanganyiko, kabla ya kununua kwa ajili ya kiti cha kukalia mtu mmoja ili kulinda mpangilio wa marembo kutoka katika kitambaa ulichochagua.

Jaribu Kabla ya Kununua

“Njia rahisi ya kuwa na uhakika kamili juu ya vitambaa unayotaka kuitumia katika fanicha fulani —na ili kujua utajisikiaje pindi ukaapo juu yake—ni kwenda na kitu ulichokiona dukani. Iwapo utapumbazwa na kitambaa ambacho hakijaoneshwa vizuri, ulizia vitambaa vya sampuli ili uweze kuoanisha na uone jinsi kitakavyoonekana baada ya kukitumia katika Fanicha yako. Iwapo utaenda na mapendekezo binafsi, hakikisha unaoneshwa sampuli kubwa ya vitambaa ili uweze kuona mwonekano wake kwa ujumla na rangi zake. Kaupekuzi makini kadogo kanaweza kukusaidia kuepuka mishangazo na kutoridhika pindi utakapoona fanicha yako inafikishwa mlangoni kwako.

 

Chagua kwa Makini kitambaa ukipendacho

Ufikapo katika Duka la WOP au Showroom zetu, wahudumu wetu watakusaidia kukuonesha na kuchagua vitambaa uwapo hapo dukani. WOP pia ina mafundi wazuri wa sofa na ushonaji, wenye ujuzi wa hali ya juu wa sofa aina zote. Jitajidi kuangalia vitambaa vyetu mchanganyiko mchanganyiko, mfano vitambaa vya maua, vitambaa vya rangi zilizochangamka na zilizopoa, na zote hizo zinapatikana WOP katika ubora wa hali ya juu.